Header Ads

Breaking News
recent

PENZI LA SIKU_SEHEMU YA TANO






PENZI LA SIKU(5)
Mtinzi:KING SOKA
0717758864
DAR ES SALAAM



Mtafaruko mkubwa ulitokea baina yangu na ndugu yangu.
Nilijiuliza kisa cha yote haya ni msicha nisiye mjua wala kunijua.
Nilifikiria sana hapa hata sijaongea nae tayari inesha kuwa tafurani hivi je akinikataa sindo nitaenda jela kwa kesi ya mauaji au akinikubali nilifikiria sana baada ya kufikiria kwa muda mrefu nilijiona mimi ndiye mwenye makosa hivyo niliona ni vyema kumuomba msamaha ndugu yandu.
Hakika hasira hasara kweli niliamini bila sababu nilimchukia ndugu yangu, na mbaya zaidi sijala mchana na hata usiku pia sijala. Yote kisa msichana ananitesa hivi hapo hapo badae anakuja kunikataa nilijikuta nikiwaza adi machozi yakinitoka.
Ni kwa mara ya kwanza nilidondosha chozi kwa kumfikiria mtu tena msicha nikifikiria na ndugu yangu nilivyo mtesa mchana milijiona ni mkosaji sana.
Sikuofia machozi bali niliofia ndugu yangu atanielewa au atakuwa kakadirika zaidi.
Mungu siyo hasumani nacho furahi ndugu yangu ni muelewa hivyo alinielewa na kunisi nijitshidi kubalansi hasira zangu.
Nilimuelewa na mambo mengne yakafuata.

Baada ya kumaliza kila kitu ikiwa pamoja na kula tuliwaaga wazee na sisi kuelekea tunapo lala. Njiani nilizidi kumsii ndugu yangu anisamehe.
"Najua nimekuudhi sana leo lakini naomba unisamehe kwa sababu ni hasira tu zile ndugu nazani atujawahi kugombana na kilicho nifanya nikuombe samahani na baada ya wewe kuniambia ulikua ukifanya utani na siyo serious niliumia sana kukukosea lakini naomba nisamehe tena ndugu na uwe nami katika safari hii maana siyo ndogo mtoto kaniteka kweli moyoni mwangu adi nakosa maamuzi sahihi utazani ndiyo mara ya kwanza napenda".
"Mwenyewe nashangaa umekuaje Jack, umebadilika gafla kiasi kwamba nilihisi labda kuna kitu nilicho kukosea tofauti na hiki maana dah! Bilia hata kosa mtu umenikasirikaia kiasi ya kufikia kidogo urushe ngumi.
Naulivyo kuwa na akili zako mbili usinge chelewa kurusha ngumi ndiyo maana ikanibidi niwe mpole tu.
Najua ndugu yangu kama kupenda umependa lakini swali ni hivi mabinti wa mjini walagahi sana angalia usije jutia upendo".
"Hilo nalifahamu lakini ndiyo hivyo tena, nimesha zama katka dimbwi la mapenzi tena gafla sana kitu ambacho ni kigeni sana na sijawahi kuwazaga hapo awali kama ipo siku nitakuja kupenda kwa stly hii".
"Hivi unavyozani ni kweli umempenda au ni hile hali umpate ukisha maliza haja zako na hamu imekuisha maana lazima twende mbele na kurudi nyuma.
Unajua nikijua hayo itakua rahisi sana mimi kupata mwangaza wa jinsi ya kukusaidia japo kimawazo".
"Yani ni hivi unaijua ndoa yani hata nikiambiwa niowe nipo tayari labda kikwazo kije dini lakini kivingne naowa kabisa aijalishi ujumu wa maisha wala nini nitakacho jali ni moyo wangu kumpata yule nimpendae basi".
"Ooooh. Safi kama kweli usemayo ni sahihi nazani ata Mungu anasikia kilio chako, hivyo ondoa shaka juu ya hilo nipe mda nitafakari kisha asubuhi nakupa jibu sahihi ya nini cha kufanya".
"Icho ndicho tunacho kosana yani wewe unalala alafu unaniambia asubuhi unipe njia ya kufanya huo sini uongo wa ajabu".
"Wewe niache nilale nitulize akili uone kama sikupi njia".
"Poa usiku mwema".
Nilibaki nikiwaza ni kweli atanipa njia rahisi ya kuanzia au ndiyo itabaki story tu.
Hatimaye na mimi nilipitiwa na usingizi

Asubuhi nilikua wa kwanza kuamka tofauti na siku zote ndugu yangu huwa wakwanza yote hiyo ni kutaka kujua jibu alilo lipata basi niliamua kumuamsha ili tu aniambia nini wazo alilo lipata.
"Baraka,Baraka,Baraka,Baraka, we Baraka!

ITAENDELEA.............


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.