Header Ads

Breaking News
recent

PENZI LA SIKU_SEHEMU YA TATU




PENZI LA SIKU   (3)
KING SOKA
0717758864
Whatsapp nk 
DAR ES SALAAM




"Sawa mbona nimekuelewa sana mkubwa, kwa hilo ondoa shaka na pigia mstari yule ndiyo shemeji yako. Naimani na kwa uwezo wa mungu. Nimempenda kutoka moyoni na nitampenda cha msingi uniombee urahisi wa kummiliki na mimi nijiite mwenye baati na kusahau yaliyo pita".
Nilibaki nikiwaza nimpigie au nimtumie text, pia nilijifikiria hata nikimpigia mida hile hile ikiwa ndiyo wameondoka hata kwao hawajafika nitamueleza nini !
 Si ataniona kama nilikua na shida ya kuchukua namba yake kwa mambo mengine na siyo kibiashara, na kufanya niaribu biashara na kufanya watu waone kama tunatumia biashara yetu kulagai wadada, hata kesho ikitokea mteja kaja afahamini ongeshindikana kuchukua namba japo ni moja ya sheria za ofisi.
 Nilizidi kuumiza kichwa bila majibu lakini nilijitahidi nisimpigie wala kumtumia text ingawa moyoni nilikua nikiumia nilitamani hata nimtafute tu na nimuulize hata jina basi na roho yangu irizike.
 Lakini bado nilishindwa na kujikuta katika mabano nikiwa sijui wapi nianzie.

 "Namba ninayo lakini nifanyaje nayo sasa.
 Nikimtafuta leo, uenda akanihisi mimi malaya au ndiyo mtindo wangu wa kuchukua namba na hiyo itapelekea kumkosa kabisa.
 Na mimi ndiyo hivyo kasha ingia moyoni kutoka ipo kazi ya ziada"
 . Nilibaki katika mabando nilizidi kuumiza kichwa bila kujua nini hatima ya mawazo hayo yote bado mawazo ayakuishia hapo kichwani nilikua na kimuemko kilichokuwa kikinisukuma nimpigie au nimtumie hata text. Basi ndani ya moyo pakawa na ushindani mkubwa huku lananiambia nipige, huku upande mwingine ukinikataza kufanya hivyo.
Lakini siku zote katka ushindani ni lazima upande mmoja ushinde hapo ndipo likanijia wazo.

 "Wewe nini jina ajakutajia mpigie umuulize jina na baada ya hapo mambo mengine yatafuata".
 Ni moja ya sauti niliyoisikia misili ya mtu akinishauri kumbe ilikua ni akili yangu tu imesha zama katka dimbwi zito la mapenzi.

Nilibaki na mawazo kiasi kwamba hata kula sikutamani nikiangalia namba ninayo kupiga nashindwa, najikuta nikipata hasira adi meno yanatetemeka na mwili mzima kwa asira ambazo ata ninaye mkasirikia simjui.
 Kwa mda wote nikikua nimekaa chini nikitafakari bila majibu. Siku hiyo nilishinda kwa tabu sana maana hata mteja aliekuja bado nilishindwa kumuudumia vizuri kutokana na mawazo niliyo kuwa nayo.

 "Kaka mambo".

 "Poa! Karibu".

 "Asante, samahani kwa kukusumbua coz nakuona upo katika dimbwi la mawazo, unawaza nin hivyo kaka angu maana nimesimama hapa lakini hata ustuki kulikoni jamani".

 "Hamna mbona nipo kawaida dada angu, karubu si unajua mawazo kawaida".

 "Kweli mawazo kawaida lakini kwako yamezidi yani mpaka unatia huruma.
 Halafu ndugu yako anakuangalia tu jamani adi uruma". Nilijitahidi kuficha uzuni kwa kujilazimisha kucheka lakini nilishindwa ilinibidi niwe mpole na nijichangamshe tu kusudi nimrizishe mteja
"Hapana mbona nipo poa dada wasiwasi wako tu".
 "Hapana sikubaliani na wewe kwa kweli mtu adi macho yamebadilika kabisa".
 "Dada bana yani uamini kabisa kama nipo sawa, nani ni hivi mimi uwa ni mgonjwa wa macho sasa na huo mwanga wa computer uwa unaniumiza macho, ndio sababu macho yapo ivi ata hivyo nilikua nimelala"

. "Hahahahahahaha! Eti mgonjwa wa macho we sema umesha korofishana na wifi uko sasa unajishauri jinsi ya kumuingia tena maana nyie wanaume looh".


ITAENDELEA.......

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.