Header Ads

Breaking News
recent

NI WAPI NILIPO KOSEA_SEHEMU YA PILI


NI WAPI NILIPO KOSEA

Mtunzi:KING SOKA

Tel:+255717758864

SEHEMU YA PILI(2)

ILIPO ISHIA.................

Breki ya kwanza,ilikua ni kwa kina Rashidy.
 Nilishangaa pale nilipofika nyumbani kwao, na kumuulizia na kuambiwa tokea jana hajarudi nyumbani. "Ajarudi nyumbani, inamaana alilala wapi?".
 "Au atakuwa kwa kina babuu?".
 Nilijiuliza maswali mengi, kichwani bila kupata majibu

. SONGA NAYO SASA.....



Niliamua kuondoka, bila kuaga moja kwa moja, safari ya kwenda kwa kina babuu ilianza.
Nilitembea kwa dakika kadhaa, nikawa nineshafika nyumbani kwa kina Babuu.
"mambo".
 "poa karibu".
 "Asante samahani Babuu yupo?".
 Nilimuuliza Dada yake baada ya kufika nyumbani kwao.
 "Yupo chumbani kwake, chumba chake kile pale.
 "Sawa ngoja nimuangalie".
 Niliondoka kuelekea, katika chumba cha Babuu
. Nilipiga hodi, akatoka njee baada ya salamu nilimuuliza kama Radhidy yupo kwao.
 "Ndio alilala apa, lakini nimeamka sijamkuta sijui kaelekea kwao sina uakika sana maana ajaniaga"
. "Poa bana, nilikuwa na shida naye maana jana kuna vitu alikua anataka kuniambia lakini tokea tuktoke mpirani sijamona nimeenda kwao ayupo sasa cjui yupo wapi?".

 "Pole jackson, lakini kuwa na subira, kwani ni jambo la muhimu sana, hadi unakuwa na wasiwasi ivyo au kumtafuta kiasi hicho?".
 "Ndio kuna vitu, anataka kuniambia, lakini sijui ni nini na hanachotaka kuniambia, hivyo ndo maana namtafuta".
Ilikua ni saa sita na dakika47, niliposikia habari iliyo niacha kinywa wazi, na kama siamini nilicho sikia Nilipata habari, iliyo nistua sana na kuniacha na sintofahamu kichwani
. Nilipokea tarifa ya kifo cha Rashidy.
 "Rashidy huyu huyu, au Rashidy gani?
 Ina maana tatizo lake ni kubwa kiasi gani hadi hafikie maamuzi ya kukatisha uhai wake?


                                     *********************** *************

 Masikini mwanangu, nini kimemkupata, jamani mimi nitakuwa mgeni wa nani katika dunia hii kwanini mimi kila siku jamani nimemkosea nini Mungu mimi, mpaka haniadhibu kiasi hiki?."
 Mwanangu juzi tu kamaliza fom four,
Nilitegemea ndio mkombozi wangu, leo kamfuata kaka yake.
 Tena kwa kifo cha ajabu namna hii,
 Ni sauti ya mama Rashidy, aliekuwa alikilia, kulamu na maswali mengi akijiuliza amemkosea nini,
 Mungu wake
. Aliendelea kulia sana, majirani wakiwa na kazi ya ziada ya kumfariji maana alikua akilia bila kupumzika. Taharifa za msiba wa Rashidy, zilienea kwa kasi kutokana na umaarufu wa wazazi wake dakika chache badae watu walishaanza kuja nyumbani apo kwa wingi.
 "Basi Dada usilie sana, tutakuwa pamoja katika kipindi hiki kigumu, usijisikie uzuni sana kila jambo uja na makusudio yake jikaze Dada yangu".
 Hatimae ndugu kutoka sehemu mbali mbali, walikua wakija na kuendelea kumfariji(wifi,shemeji yao)
 Wakati wote nilikua ni kama siamini, kila rafiki yangu niliekuwa nikimwambia alibaki na butwaa
. Akuna alie amini na aikuwa rahisi kuamini.
 "Jackson ivi ni kweli au utani tu, maana watu kwa kuzusha si unakumbuka juzi kati walivyo zusha kwa yule mzee wa bondeni?". Nakumbuka lakini hili ni kweli, binafsi kwa upande wangu najilazimisha nisiamini"
 "poa bana, mimi ngoja niende niwape tarifa washikaji, jembe limetutoka hivi hivi kweli siamini?"
. "Lakini yule mama anapitia wakati mgumu sana, juzi juzi mume kafariki ajakaa sawa kijana wake leo tena mtoto wake kwa kiume ukizingatia ndo kamaliza fom four, hata mwezi bado tokea amalize jamini".
"Mmmmmmmmh Mama happy tusijadili sana, tutaonekana wambea maana nilicho sikia kinasikitisha kuhusiana na hiki kifo cha Rashidy". "kwani kuna nini?".

 

Itaendelea........


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.