Header Ads

Breaking News
recent

PENZI LA SIKU_SEHEMU YA PILI




 

PENZI LA SIKU(2)

KING SOKA
0717758864



Baada ya kuondoka nilibaki na ndugu yangu. Huku nyuma nilikua na kazi ya kujibu maswali kutoka kwa ndugu. Halikasirishwa na kitendo cha mimi kutoa Cd bure, baada ya kugundua kuwa amekasirika ilinibidi nijishushe chini na kuwa mpole. Niliamua kumuomba msamaha na kumueleza hali alisi alinielewa lakini bado akurizika na majibu

. "Poa nimekueleea ndugu ondoa shaka bana".
 Aliniambia lakini alionekana bado yupo na hasira ndipo nilipo muuliza mbona kama umesamehe lakini bado una asira. Ndipo alipo niuliza hivi mimi naakili au natumia maji nilijiuliza sana bila jibu ndipo niliamua kumuliza tena.

 "Umesemaje ndugu".
 Alirudia swali lake ambalo liliniuzi sana na kuamua kuondoka kwa hasira.
 "Haiwezekani anitukane kisa cd ya1000 ndo anambie na tumia maji katika kichwa changu hizi zarau mimi sikubaliani nazo au ni wivu umemjaa tu, anaona kama mimi nitafaidi kumpata mtoto pini kama yule, maana watu wengine wanawivu wa kiukoo labda ndiyo tatzo lakr na huyu ndugu yangu, uwezi mzarau mtu kisa cd ya1000 pengine ana lake moyoni".
Niliwaza sana nikiwa na hasira niliamua kurudi tu kwa kuwa nilikuanikitazama movie nilirudi kuendelea na movie yangu uku nikiwa nimevimba mashavu kwa hasira. Alijua nimekasirika na kazi ya kuniomba msamaha iliamia kwake wakati mda mfupi tu nilitoka kumuomba yeye samahani kwa kutoa cd bure ikiwa kama kufidia cd waliyo ichukua ikawa inaskrach.

 "Nisamehe ndugu yangu coz sijaongea hivyo labda kwa maana ya nimekuzarau au laah, hapana niliongea na sikujua kamanaweza kukuuzi, hivyo nisamehe bana".

 "Poa mbona mimi nipo fresh! We si uliona mimi natumia maji barida tu".
  "Hapana ndugu tuyamalize sisi ndugu kulumbana haina tija kizuri nikukaa na kujadili maisha njinsi yatakavyo kuwa na siyo muda wa kubisha na kulumbana".
 "Sasa kumbe wayajua hayo! Mbona sasa unakuwa unanizarau kisa1000 mi siku ukirudi nizarau hivyo kiru, tunamalizana kiaina".
 "Sawa lakini naomba nikuulize kusudi nijue kama ni kweli au utani".
 "We uliza tu nakujibu".
 Niliamua kustopisha movie kumsikiliza na maswali yake maana nilisha jua bado atsrudi pale pale tulipo tokea.
 Hivyo nilijiweka tayari kwa kupokea maswali kama nipo kituo cha polisi maana mmmh Cd imezua jambo dadeq.

 "Hivi ni kweli yule binti umempenda kama ulivyo sema, na ukimpata upo tayari kutangaza ndoa. Maana nakuwa kama sijakuelewa vizuri. Au ulikua ukinitania tu ndugu yako maana wewe sikuelewi elewi mtu umemuona siku moja tu".

 "Yap! Yani nikimpata tu na ndoa naanzisha na siyo kumchezea na kisha kumuacha nimempenda kiukweli uwezi amini ata mimi najishangaa kwa nini imenitokea hivyo lakini sijui atanipokea vipi mimi mtoto wa watu miye".
 "Hahahahahahaha! Ndugu sasa unaanza kudata siyo bure yani hata sababu ya wewe kumpenda auijui au ndoyo hile kutuficha sisi tusijue kumbe nyuma ya pazia mwafanya mambo.
 Kuwa muwazi bana nijue na mimi nimtambue shemeji yangu. Mwenywe binafisi nimemkubali mtoto mzuri na anasifa zote.
 Japo leo ni kwa mara ya pili namuona lakini kiukweli nimemuelewa sana hivyo fanya kweli.
 Mwenyewe inaelekea kakuelewa ndiyo maana ata alikua akicheka kwa aibu sana uku akitazama pembeni. Penzi la kweli lipo pale na utulie nae ukimpata sawa kijana".

ITAENDELEA......

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.